wapiganaji hao ambao ni wafuasi wa madhehebu ya Sunni ambao pia wanapigana na serikali ya syria wamefanya mashambulizi makali yaliyopelekea maelfu ya wananchi kukimbia na kuacha miji yao.
wapiganaji hawa wanadai kuwa wanaojulikana kama Daesh wadai wanataka kutengeneza dola la kiislamu litalokusanya nchi mbili za Iraq na Syria.
Daesh wamekuwa wakifanya jinai na unyama wa kupindukia hasa huko Syria ambapo hawakumhurumia mtoto, mwanamke wala mzee bali husafisha kila wanachoona ni kikwazo mbele yao.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon ameelezea kusikitishwa sana na hatua ya wapiganaji wa Daesh wenye mfungamano ya wazi na al Qaida ya kuudhibiti mji wa Mosul.
jeshi la Iraq limeahidi kuukomboa mji huo mapema iwezekanavyo.
11 Juni 2014 - 07:04
Msimbo wa Habari: 615138
wapiganaji wa kiislamu wenye misimamo mikali wameteka mji wa Mosul nchini Iraq jana baada ya mapambano shadidi.